spacer
spacer spacer spacer spacer spacer spacer spacer spacer spacer spacer
spacer
spacer
spacer
spacer
Siri Zangu | Swahili Net | Swahili Fire | Mapenzi Ngono na Ndoa
spacer

Thursday, April 21, 2011

Mashairi Kutoka Tanzania:Zawadi

Amesema Yarasuli, maneno yalo muruwa,
Tena ambayo ni kweli, matamu kama haluwa,
Kwa Jamila na Jamali, bila hata kubaguwa,
Mapenzi zinazidisha, zawadi mkipeana.

Waja inasitahili, kufanya bila ya ngowa,
Na wala si ukatili, jambo la kusisimua,
Toa bila ya ukali, wala hutopungukiwa,
Mapenzi zinazidisha, zawadi mkipeana.

Uondoshe ubakhili, hilo jambo ukijuwa,
Usihofu yako mali, kwa zawadi kuitowa,
Kabana yake Kabuli, kingi utazidishiwa,
Mapenzi zinazidisha, zawadi mkipeana.

Usione mushikeli, bali jambo lilo sawa,
Ukaufanya muhali, hodari wa kuvumbuwa,
Ni akiba iso mbali, nawe wajakutendewa,
Mapenzi zinazidisha, zawadi mkipeana.

Wema huwa ahu'feli', nahau yangu dokowa,
Bora huu muhimili, upende kama mauwa,
Weka kwenye jeduwali, fakiri na wenye hatuwa,
Mapenzi zinazidisha, zawadi mkipeana.

Beti sita kituoni, mbele sitoendelea,
Amini usiamini, wasia huu mbolea,
Tena ulio yakini, Mtume aloongea,
Mapenzi zinazidisha, zawadi mkipeana.

0 comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home

CelebSense

Loading...
spacer
 
gipoco.com is neither affiliated with the authors of this page nor responsible for its contents. This is a safe-cache copy of the original web site.